Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza Arafi, mkurugenzi wa hawza nchini, katika mkutano na wakurugenzi wa idara za kitaifa na mikoa za Masuala ya Wanafunzi na Wahitimu wa hawza, uliofanyika katika Hawzah ya Ma‘sumiya huko Qom Iran, alisema katika maelezo yake huku akitoa rambirambi kwa kipindi cha Fatimiyya na kuipongeza idara ya Masuala ya wanafunzi kwa maandalizi ya kongamano hili. Alihakikisha: uwepo wa Hujjatul Islam wal-Muslimin Qanavati katika nafasi hii ni muhimu kutokana na fadhila zake binafsi, uzoefu wake wa uongozi na ufahamu wa hali halisi za hawza.
Mkurugenzi wa hawza alitoa maelezo yake katika mitazamo mikuu miwili:
Mtazamo wa kwanza: Mfumo wa kutoa huduma katika Uislamu
Maana ya Huduma katika Uislamu na Kutosheleza Mahitaji
Ayatullah Arafi alisema kuwa; huduma katika Uislamu ina mfumo mpana na wa kimantiki, akibainisha: Huduma ni kutosheleza mahitaji ya wengine na kutoa matokeo yanayohitajika na mtu binafsi au jamii kwa ngazi na viwango tofauti. Maana hii inatambulika pia katika mafundisho ya Kiislamu na imethibitishwa na maelezo mbalimbali ya maneno kama vile maneno ya Imam Swadiq (as) yasemayo:
"قَضَاء حَاجَة اَلْمُؤْمِنِ أَفْضَلُ مِنْ أَلْفِ حِجَّةٍ مُتَقَبَّلَةٍ بِمَنَاسِکِهَا وَ عِتْقِ أَلْفِ رَقَبَةٍ لِوَجْهِ اَللَّهِ وَ حُمْلَانِ أَلْفِ فَرَسٍ فِی سَبِیلِ اَللَّهِ بِسُرُجِهَا وَ لُجُمِهَا.""Kukidhi haja ya mu’min ni bora kuliko hijja elfu moja zilizokubaliwa kwa ibada zake, na kuwakomboa watumwa elfu moja kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na farasi elfu moja na kamba zake katika njia ya Allah."
[Mishkat al-Anwar fi Ghurar al-Akhbar, J.1, uk. 143]
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Hawza aliongeza: Katika rasilimali za lugha, huduma inamaanisha pia al-qiyam bi-Hawajil-Nas — yaani kushughulikia mahitaji ya watu. Kwa kuwa haja na mahitaji yana vipimo na viwango tofauti, huduma pia inakuwa na aina na viwango mbalimbali.
امام کاظم علیه السلام:
"إنَّ لِلّهِ عِبادا فِی الأرضِ یَسعَونَ فی حَوائجِ النّاسِ هُمُ الآمِنونَ یومَ القِیامَةِ"Imam Kazim (a.s) anasema: "Hakika Mwenyezi Mungu ana wafuasi katika dunia ambao wanajitahidi kutimiza mahitaji ya watu; hao ndio watakaopata usalama siku ya Kiyama."
[Al-Kafi, J.2, uk. 197]
Aina za Mahitaji: Binafsi na ya Kijamii
Ayatullah Arafi akiashiria uainishaji wa mahitaji ya binadamu, alisema: Baadhi ya mahitaji ya binadamu ni binafsi na ya ndani, na baadhi mengine yana mtazamo wa kikundi. Jamii yenyewe, kama kiumbe hai, ina mahitaji halisi yanayozidi mahitaji ya mtu binafsi, na kutimiza mahitaji hayo ni ishara ya maisha ya kijamii.
Ngazi tatu za kutimiza mahitaji
Mkurugenzi wa hawza alisema: Kutimiza mahitaji kuna ngazi tatu:
1. Kuitambua haja;
2. Kuelewa au kuhisi haja;
3. Kuomba kutimizwa kwa haja.
Ayatullah Arafi aliongeza: Wakati mwingine binadamu anahitaji kitu lakini hajui kuhusu kitu hicho, kama mgonjwa aliyepoteza fahamu anayehitaji matibabu lakini haelewi hali yake. Kutimiza haja kama hiyo pia ni huduma. Ngazi ya juu zaidi ni pale ambapo mtu anaelewa haja yake na anaumia kutokana na kutokuwa nayo. Huduma katika ngazi hii, zaidi ya kutimiza haja, hupunguza maumivu na huleta furaha.
Kutokana na mtazamo huu, mahitaji yanagawanywa katika makundi matatu:
1. Haja halisi: kabla ya mtu kuifahamu;
2. Haja iliyoeleweka: kwa kuelewa na kupata maumivu;
3. Haja iliyobainishwa: kwa kuomba na kuhitaji msaada.
Kumuhitajia Mwenyezi Mungu, ndio Kichwa cha Mahitaji yote
Mwalimu wa masomo ya fiqh na usul hawza ya Qom, akirejelea nadharia ya ngazi za mahitaji katika saikolojia ya kisasa, alisema: Uislamu unakubali mpangilio huu kwa ujumla, lakini unasema kuwa juu ya yote kuna haja ya Mwenyezi Mungu. Kama Qur’an ilivyoeleza katika Aya ya 15 ya Surah Fatir:
يَا أَيُّهَا النَّاسُ أَنتُمُ الْفُقَرَاءُ إِلَى اللَّهِ وَاللَّهُ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ
"Enyi watu! Nyinyi ndio wenye haja kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha, Msifiwa."
Mkurugenzi wa hawza alisisitiza: Kimsingi katika mafundisho ya Kiislamu, kumuhitajia Mungu ndio asili ya mahitaji yote, kwani baraka za Mwenyezi Mungu ndizo zinazoumba utu wa binadamu na pia hutoa kamilifu zake.
Thawabu Kubwa ya Huduma Kulingana na Mafundisho ya Kiislamu
Ayatullah Arafi akirejelea usemi wa Imam Sadiq (a.s) alisema:
قَالَ اَلصَّادِقُ عَلَیْهِ اَلسَّلاَمُ: قَضَاء حَاجَة اَلْمُؤْمِنِ أَفْضَلُ مِنْ أَلْفِ حِجَّةٍ مُتَقَبَّلَةٍ بِمَنَاسِکِهَا وَ عِتْقِ أَلْفِ رَقَبَةٍ لِوَجْهِ اَللَّهِ وَ حُمْلَانِ أَلْفِ فَرَسٍ فِی سَبِیلِ اَللَّهِ بِسُرُجِهَا وَ لُجُمِهَا
Imamu Swadiq (amani iwe juu yake) alisema: Kutimiza haja ya muumini ni bora kuliko hija elfu moja zilizokubaliwa pamoja na matendo yake, na kuwakomboa watumwa elfu moja kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na farasi elfu moja waliobeba mizigo, waliopambwa kwa matandiko na hatamu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Imamu Swadiq (amani iwe juu yake) pia anasema: Hakika kutimiza haja ya muumini ni kwa yakini bora kuliko hija moja, na hija nyingine, na hija nyingine… na Mtukufu alihesabu hadi hija kumi.
[Mishkat al-Anwar fi Ghurar al-Akhbar, Juzuu ya 1, uk. 143]
Baada ya kueleza thawabu za kufanya tawafu alisema: Kutimiza haja ya muumini ni bora kuliko kufanya tawafu mara kumi. Hili linaonesha kuwa; kuondoa huzuni kutoka moyoni mwa muumini au kupanda mbegu ya furaha moyoni mwake kuna nafasi ya juu sana.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Vyuo vya Kiislamu aliongeza: Katika vyanzo vya riwaya kama vile vitabu vinne na Wasail al-Shia katika milango ya kufanya mema na kutimiza haja za waumini, kuna upeo wa kushangaza wa thawabu za kuhudumia; kutoka kutimiza mahitaji ya mali hadi kuhakikisha utulivu wa kiroho.
Mabawa mawili ya ufanisi: Ibada na huduma
Mjumbe wa uongozi wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi wa Kiislamu alisisitiza kuwa; huduma ni sehemu isiyotenganika na njia ya ufanisi wa mwanadamu, akasema: Uislamu unamchukulia mwanadamu kama kiumbe anayeihitaji mabawa mawili ili kufikia ukamilifu:
Kwanza: Ibada na kumwabudu Mwenyezi Mungu kwa ndani;
Pili: Huduma na kushiriki kijamii kwa nje.
Ayatollah Arafi aliongeza: Mwanadamu kamili kwa mtazamo wa Uislamu ni yule anayekamilisha vipengele hivi viwili kwa pamoja; si yule aliyejifungia katika ibada wala asiyejali jamii.
Utambulisho wa asili wa Hawza: Kutoa huduma
Mkurugenzi wa vyuo vya Kiislamu kote nchini Irani alisema kuwa; utambulisho wa asili wa hawza ni kutoa huduma, na akaeleza: Hawza ina vipengele viwili vya msingi: Kwanza, uelewa wa kina wa elimu za dini na kunufaika na Kitabu na Sunna; Pili, kuwa na mtazamo wa kijamii.
Akinukuu kauli ya Kiongozi Mkuu kuhusu hawza kuwa na mtazamo wa nje, alisema: Ikiwa siku moja tutakuwa na hawza iliyojaa fiqhi na fikra ya kiakili, lakini isiyokuwa na nafasi katika kusambaza na kuyatekeleza hayo, basi hawza hiyo itakuwa imepoteza utambulisho wake halisi.
Huduma ya kiakili na kimaadili, kilele cha hawza
Mjumbe wa Baraza Kuu la hawza alisisitiza kuwa; huduma kuu ya hawza ni huduma ya kiakili na kimaadili, na akaongeza: Makundi ya jihadi na huduma za uwanjani ni zenye thamani, lakini huduma ya kweli na ya mbinguni ni kuwasilisha fikra ya kimungu kwa mwanadamu na kujibu kiu ya kiroho na kiakili ya mwanadamu.
Misingi minne ya msingi ya utoaji huduma wa Kiislamu
Mkurugenzi wa vyuo vya Kiislamu nchini Iran, alisema kuwa; Uislamu una mfumo wa fikra uliopangika katika kila mada, na akaeleza: Kuhusu kila uwanja, kuna aina tatu za fikra: “fikra ya kimantiki na kifalsafa”, “fikra ya kifiqhi”, na “fikra ya kimaadili”.
Ayatollah Arafi aliendelea na kutaja misingi minne ya msingi ya mfumo wa utoaji huduma katika Uislamu kama ifuatavyo:
Msingi wa kwanza: Mtazamo wa kimungu kwa kiumbe
Mtume Mtukufu (rehma na amani ziwe juu yake na Aali zake), Imamu Swadiq (amani iwe juu yake):
عَلِیُّ بْنُ إِبْرَاهِیمَ عَنْ أَبِیهِ عَنِ اَلنَّوْفَلِیِّ عَنِ اَلسَّکُونِیِّ عَنْ أَبِی عَبْدِ اَللَّهِ عَلَیْهِ اَلسَّلاَمُ قَالَ قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّی اَللَّهُ عَلَیْهِ وَ آلِهِ : اَلْخَلْقُ عِیَالُ اَللَّهِ فَأَحَبُّ اَلْخَلْقِ إِلَی اَللَّهِ مَنْ نَفَعَ عِیَالَ اَللَّهِ وَ أَدْخَلَ عَلَی أَهْلِ بَیْتٍ سُرُوراً
Alī bin Ibrāhīm kutoka kwa baba yake kutoka kwa al-Nawfalī kutoka kwa al-Sakūnī kutoka kwa Abī Abdillāh (amani iwe juu yake) alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani ziwe juu yake na Aali zake) alisema: “Viumbe ni familia ya Mwenyezi Mungu, na kipenzi zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni yule anayeinufaisha familia ya Mwenyezi Mungu na kuingiza furaha katika familia moja.”
[al-Kāfī, Juzuu ya 2, uk. 164]
Kwa hakika msingi wa kwanza na wa kina kabisa ni kwamba mwanadamu ajue kuwa kila anapomhudumia mwingine, kwa hakika anamhudumia Mwenyezi Mungu. Katika hadithi hii maarufu imesemwa: “al-khalqu ‘iyālullāh” (viumbe vyote ni familia ya Mwenyezi Mungu). Mkono wa mwenye haja ni kivuli cha mkono wa Mungu.
Msingi wa pili: Kuhifadhi heshima ya hadhira
Yule anayepokea huduma ana heshima ya asili. Mtoa huduma anapaswa kuona na kuhisi heshima hii si kwa maneno tu, bali pia kwa moyo wake. Kwa mabadiliko madogo tu ya mwili au hali, nafasi hubadilika, na mhudumu huelewa kuwa ubora wote ni amana kutoka kwa Mungu.
Msingi wa tatu: Huduma isiyo ya kibiashara ya kidunia
Mkurugenzi wa vyuo vya Kiislamu nchini Iran, alitaja aya ya 9 ya Surah al-Insān:
“إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللَّهِ لَا نُرِیدُ مِنْکُمْ جَزَاءً وَلَا شُکُورًا”
Akasema: Katika mantiki ya Uislamu, huduma si biashara ya kidunia. Ukamilifu wa huduma ni kuiona kama biashara na Mungu, si na wanadamu.
Mwalimu wa masomo ya juu ya fiqhi na usūl katika chuo cha Qum aliongeza: Mhudumu wa kweli hafanyi kazi yake kwa ajili ya ujira, cheo au thawabu ya kidunia, bali nia yake ni radhi za Mungu. Amīrul-Mu’minīn (amani iwe juu yake) alisema: “Naapa kwa Mungu, sikuchukua hata hatua moja kwa ajili ya utawala.”
Pia alimwambia Ibn Abbas:
«مَا قِیْمَهُ هذَا النَّعْلِ؟ فَقُلْتُ: لَا قِیْمَهَ لَهَا، فَقالَ (علیهالسلام): وَ اللهِ لَهِیَ أَحَبُّ اِلَیَّ مِنْ إمْرَتِکُمْ، إلّا أنْ أقیمَ حَقّاً، أوْ أدْفَعَ باطِلاً»
“Ni ipi hamani ya kiatu hiki?” Nikasema: “Hakina thamani.” Akasema: “Naapa kwa Mungu, hiki ni kipenzi kwangu kuliko utawala wenu, isipokuwa tu ikiwa nitatekeleza haki au kuondoa batili.”
[Nahjul-Balagha, Khutba ya 33]
Hii ndiyo roho ambayo, iwapo mtu ataweza kusema: “Kila nifanyalo kwa ajili ya mwanafunzi, mwalimu, mfumo na hawza, si kwa ajili ya pesa, si kwa ajili ya cheo, si kwa ajili ya daraja, si kwa ajili ya heshima, si kwa ajili ya pongezi wala shukrani,” basi huyo amefikia kilele cha kutoa huduma katika Uislamu.
Thamani halisi ya mwanadamu na kazi yake inategemea kiwango hiki cha “ikhlasi na kutokuwa na madai.” Hatupaswi kuuza “maisha” na “uwepo” wetu kwa thamani ndogo. Uwepo wa mwanadamu una thamani ya juu zaidi; thamani yake halisi ni “radhi za Mwenyezi Mungu” tu.
Msingi wa nne: Mfumo wa vipaumbele
Ayatollah Arafi alisisitiza: Kadiri huduma inavyoelekezwa kwenye masuala ya msingi na ya kina zaidi, ndivyo inavyopata thamani ya juu zaidi. Kutoa kipaumbele kwa huduma kwa mujibu wa maslahi ya jumla na mahitaji ya jamii ya kidini ni miongoni mwa vigezo vya msingi.
Mtazamo wa pili: Matarajio kutoka kwa wasidizi wa masuala ya wanafunzi
Dokezo la kwanza: Uelewa wa mifumo ya kielimu na mipango ya mabadiliko
Mkurugenzi wa vyuo vya Kiislamu nchini Iran, alisema: Masuala ya wanafunzi na wahitimu yanapaswa kupanga huduma zao kwa mujibu wa mifumo ya kielimu, ya masomo na ya kulinganisha, na kuwa na uelewa wa aina ya kazi na programu za mifumo hiyo.
Huduma inayolenga mifumo ya msingi ya ukuaji wa elimu na imani ina ubora zaidi kuliko huduma za juu juu na za muda mfupi. Katika usimamizi wa Kiislamu, “kutoa kipaumbele katika huduma kwa mujibu wa maslahi ya jumla na mahitaji ya jamii ya kidini” ni mojawapo ya vigezo vya msingi. Kwa mtiririko huo, mhimili wa pili wa mijadala yetu unahusiana na “matarajio na mahitaji ya hawza kutoka kwa wahudumu wake.”
Matarajio haya yanatokana na maelezo rasmi ya majukumu na maamuzi ya mipango ya hawza.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza alitaja majukumu makuu matano ya hawza kama ifuatavyo:
1. Kulea nguvu kazi kupitia elimu
2. Kuzalisha elimu na maudhui kupitia utafiti
3. Kumkuza mtu mwenye imani ya kidini
4. Kuhubiri na jihadi ya ufafanuzi
5. Usimamizi wa kidini na utekelezaji wa maadili ya kimungu katika jamii
Ayatollah Arafi alisisitiza: Kila huduma inapaswa kuwa na wazo hili akilini mwetu kwamba inahusiana na lengo lipi kati ya haya. Matokeo ya mwisho yanapaswa kuwa mwanachuoni, mwalimu, mtafiti, mhubiri au meneja wa kitamaduni ambaye ni kiongozi wa jamii kuelekea malengo ya ustaarabu wa Kiislamu.
Maoni yako